Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Sunday 9 June 2013

18 wauawa katika mapigano Kismayo, Somalia

                                 

 
Watu 18 wameuawa katika mapigano makali baina ya makundi hasimu ya wanamgambo wanaopigana kuudhibiti mji wa Kismayo kusini mwa Somalia.
Kwa mujibu wa wakaazi wa mji huo, watu 13 waliuawa jana Jumamosi na wengine siku ya Ijumaa. Imearifiwa kuwa wanamgambo wa Ras Kamboni wamechukua udhibiti wa eneo la Calanleey mjini Kismayo. Wanajeshi wa Umoja wa Afrika kutoka Kenya ndio wanaosimamia usalama katika bandari muhimu ya Kismayo na maeneo ya karibu. Oktoba mwaka 2012 wanajeshi wa Kenya wakiungwa mkono na wanamgambo wa Ras Kamboni walichukua udhibiti wa Kismayo kutoka kwa wapiganaji wa al-Shabab. Afisa mwandamizi wa al-Shabab mjini Kismayo Sheikh Xudayfa Abdirahman amedai kuwa Kenya ndio iliyochochea mapignao ya hivi karibuni.
Baadhi ya wanasiasa wa serikali kuu ya Somalia wanadai kuwa Kenya inataka kueneza satwa yake katika eneo la Jubaland ambalo mji wake mkuu ni Kismayo. Hivi karibuni eneo hilo lilijitangazia mamlaka ya ndani na kumteua Ahmed Mohamed Madoobe kama rais wake. Wakuu wa Mogadishu wamebainisha upinzani wao kwa hatua hiyo.

0 comments:

Post a Comment