Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Saturday, 25 May 2013

Zaidi ya asilimia 25 ya wananchi A/Kusini hawana kazi

                                       15 Rajab,1434 Hijiriyah/ May 25,2013 Miyladiyah
 Taasisi ya Utafiti ya Afrika Kusini imetangaza kuwa, zaidi ya asilimia 25 ya wananchi wa nchi hiyo hawana kazi. Taasisi hiyo imetangaza kuwa, kiwango sahihi cha watu wasiokuwa na kazi nchini humo ni zaidi ya asilimia 25. Taasisi hiyo imeeleza kuwa, miezi mitatu ya mwanzo ya mwaka huu wa 2013 inaonyesha kuwa , kiwango cha watu wasio na kazi kiliongezeka  kwa watu  laki moja, na kufikia watu milioni nne na laki sita. Wataalamu wa kiuchumi wa Afrika Kusini wanaeleza kuwa, kiwango cha juu cha watu wasiokuwa na kazi nchini humo ni moja ya sababu ya kuibuka mara kwa mara ghasia na machafuko nchini humo

0 comments:

Post a Comment