Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 21 May 2013

Wagombea kiti cha urais Iran watangazwa 
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Iran imetangaza majina ya watu 8 ambao wameidhinishwa kugombea kiti cha urais baada ya kuchunguzwa na Baraza la Kulinda Katiba.
Walioidhinishwa kugombea kiti cha urais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni pamoja na mwakilishi mkuu wa Iran katika mazungumzo ya nyuklia  Saeed Jalili,  spika wa zamani wa bunge Ghulam Ali Haddad Adel, kamanda wa zamani wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu Mohsen Rezai, mwakilishi wa zamani wa Iran katika mazungumzo ya nyuklia Sheikh Hassan Rohani, makamu wa zamani wa rais Mohammad-Reza Aref, waziri wa zamani wa mawasiliano Mohammad Gharzi, meya wa Tehran Mohammad Bagehr Qalibaf na waziri wa zamani wa mambo ya nje Ali Akbar Velayati.
Rais wa zamani wa Iran Sheikh Hashemi Rafsanjani na mkuu wa  Ofisi ya Rais, Esfandiyar Rahim Mashaei hawakuidhinishwa kugombea urais katika kipindi hiki.
Uchaguzi wa rais wa awamu ya 11 utafanyika Juni 14 na mshindi wa uchaguzi huo atachukua nafasi ya Rais Mahmoud Ahmadinejad anayemaliza muda wake na ambaye kwa mujibu wa katiba hawezi kugombea mara hii baada ya kuhudumu kwa mihula miwili mfululizo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Seyyed Solat Mortazavi alitoa taarifa siku ya Jumamosi na kusema kampeni zitaanza rasmi baada ya Baraza la Kulinda Katiba kutangaza orodha rasmi ya wagombea. Kampeni zitamalizika masaa 24 kabla ya kuanza zoezi la uchaguzi.
 

0 comments:

Post a Comment