Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Uingereza ametaka mgogoro wa Syria
utatuliwe kwa njia za kisiasa. Akizungumza mbele ya bunge la nchi hiyo,
William Hague ameongeza kuwa, mgogoro wa Syria hauwezi kutatuliwa kwa
njia za kijeshi na hivyo ameitaka serikali ya Damascus na makundi ya
waasi nchini humo kufanya mazungumzo ili kukomesha mgogoro nchini humo.
Hata hivyo, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Uingereza amesisitiza azma
ya London ya kuendeleza uungaji mkono wake kwa makundi ya kigaidi
nchini Syria na kubainisha kuwa, katika kikao kijacho cha Umoja wa
Ulaya, London itatoa pendekezo la kurekebishwa na kulegezwa vikwazo vya
silaha vilivyowekwa na umoja huo dhidi ya makundi ya kigaidi nchini
Syria. Matamshi ya Hague yanatolewa katika hali ambayo, Marekani,
Uingereza, Ufaransa na hali kadhalika Saudi Arabia, Qatar na Uturuki
ziko mstari wa mbele katika kushadidisha mgogoro wa Syria kwa kuyapa
misaada ya silaha na fedha makundi ya kigaidi nchini humo.
Sikiliza Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment