Rais Omar Hassan al Bashir wa Sudan amesema kuwa, Khartoum haitafanya
mazungumzo na waasi wa Muungano wa Harakati ya Kimapinduzi ya nchini
humo. Akizungumza na vyombo vya habari makao makuu ya jeshi mara baada
ya majeshi ya Sudan kuukomboa mji muhimu katika jimbo la Kordofan
Kusini, Rais al Bashir amesisitiza kama ninavyonukuu:"Kamwe hatutafanya
mazungumzo na vibaraka na magaidi ambao wenyewe wanajiita harakati ya
kimapinduzi." Harakati ya Kimapinduzi ni muungano wa makundi matatu
yaliyoko Darfur na yamekuwa yakipambana na serikali tokea mwaka 2003.
Makundi hayo matatu ni Harakati ya Uadilifu na Usawa, Harakati ya
Ukombozi wa Sudan tawi la Mini Minawi na tawi la AbdulWahid Nour na kwa
upande mwingine, Harakati ya Wananchi iliyoko kaskazini mwa Sudan nayo
imekuwa ikipambana na serikali katika mikoa ya Kordofan na Blue Nile
tokea mwaka 2011.
Sikiliza Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment