Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Saturday, 18 May 2013

Rais Pohamba wa Namibia atangaza hali ya hatari

 
Rais Hifikepunye Lucas Pohamba wa Namibia

Rais Hifikepunye Lucas Pohamba wa Namibia ametangaza hali ya hatari iliyosababishwa na ukame mkubwa unaoikabili nchi hiyo. Rais Pohamba ameongeza kuwa, ukame mkubwa unaoikabili nchi hiyo umesababishwa na kiwango kidogo cha mvua, na bila shaka utaleta taathira mbaya kwa maisha ya wananchi wa nchi hiyo. Rais Pohamba amesisitiza kuwa, ukame wa mwaka huu utaliathiri taifa lote la Namibia na kuna uwezekano mkubwa kiwango cha mavuno ya nafaka kushuka na kufikia hata chini ya asilimia 48 katika badhi ya maeneo ya nchi hiyo.

0 comments:

Post a Comment