Picha ya pamoja na watumishi wa TANROADS mkoa wa Iringa na Rais Jakaya Kikwete
Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na v iongozi wa dini mkoa wa Iringa waliosimama nyuma
Rais Kikwete akiangana na wananchi waliofika kushuhudia zoezi la uwekaji jiwe la Msingi barabara ya lami kati ya Iringa - Dodoma
RAIS
Jakaya Kikwete ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa barabara ya Iringa
- Dodoma na kuwaonya watu wanaoendelea kuhujumu miundo mbinu kwa kuiba
alama za barabarani .
Rais Kikwete alisema kuwa mbali ya
serikali kujipanga katika kuhakikisha kuwa nchi nzima inaunganishwa na mtandao
wa barabara za lami ila bado baadhi ya watu wamekuwa wakifanya hujuma
katika barabara bila kuangalia fedha ambazo serikali imetumia katika ujenzi wa
barabara hiyo na kuwataka wananchi kuwa walinzi wa barabara hizo
.
Akizungumza na wananchi wa jimbo la
Isimani katika eneo la Migoli - Mtera wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi
katika ujenzi wa barabara ya Iringa - Dodoma leo ,Rais Kikwete alisema kuwa
ili kuendelea kutunza barabara hizo ni vema wanaohujumu miundo mbinu
kufichuliwa na kuchukuliwa hatua kali.
Hata hivyo alisema mbali ya serikali
kuendelea na uboreshaji wa miundo mbinu hapa nchini bado anawataka
watanzania kutambua jitihada hizo .
Alisema kuwa sasa watanzania wanaweza
kusafiri hadi Kenya na Uganda kwa barabara ya lami na kuwa bado jitihada
zitaendelea daima.
Rais Kikwete alisema kuwa mbali ya
serikali kujipanga kwa ujenzi wa barabara bado lengo la serikali ni
kuhakikisha nchi nzima inaunganishwa kwa mtandao wa barabara ya lami na kuwa
kazi hiyo tayari imeanza.
Alisema kuwa serikali yake toka imeingia
madarakani imeendelea kuongeza fedha katika mfuko wa barabara na kuwa
lengo ni kuendelea kuongeza zaidi fedha katika mfuko huo ili kuwezesha
ujenzi wa barabara nchini kuweza kukamilika
Rais Kikwete pia amewapongeza viongozi
wa TANROADS kwa kazi nzuri wanayoendelea kuifanya na kwa mbali ya kupongezwa
bado hawapaswi kulewa sifa na badala yake kuendeleza jitihada za kusimamia
kazi hiyo kwani upo usemi unao sema kuwa mgema akisifiwa pombe huweka maji
.
Pia Rais Kikwete alimpompongeza waziri wa
fedha Dkt Wiliam Mgimwa kwa kuendelea kuidhinisha fedha kwa ajili ya miradi ya
barabara hapa nchini na kuwa bila wizara hiyo kutenga bajeti kazi hiyo
ingeendelea kuwa ngumu.
Akizungumzia kuhusu amani na utulivu nchini
Rais Kikwete alisema wapo baadhi ya watu usiku na mchana wamekuwa
wakipanga mipango mibaya ya kuvuruga amani ya nchi hii na hivyo noi vema
watanzania kuwaepuka watu wenye nia ya kuchafua nchi hii kwa kuchochea
vurugu.
Alisema iwapo watanzania watakataa
kuwasikiliza watu hao wala kushirikiana nao kamwe Tanzania haitaingia katika
machafuko yanayopangwa na watu hao wasio penda mema.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Isimani
wilayani Iringa mkoani Iringa Bw. Wiliam Lukuvi alimpongeza Rais Jakaya
Kikwete kwa kuwawezesha wakazi wa tarafa ya Isimani kuweza kuanza
kushuhudia mapinduzi makubwa ya kimaendeleo kupitia mradi mkubwa wa barabara
ya kiwango cha lami kutoka Iringa - Dodoma inayopita katika tarafa hiyo
.
Lukuvi ambae ni waziri wa nchi ofisi
ya waziri mkuu (sera na uratibu wa bunge) alisema kuwa barabara hiyo
ambayo ni ukombozi mkubwa kwa nchi za kusini mwa Tanzania ilikuwemo katika
mkakati wa kujengwa kwa kiwango cha lami kwa kitambo kirefu na kila awamu
wananchi walikuwa wakiulizana juu ya kuanza kwa mradi huo.
Hata hivyo alisema baada ya awamu hii ya
nne chini ya Rais Kikwete wananchi hao wameweza kushuhudia majibu ya
maswali yao kwa kuanza kwa ujenzi huo ambao kila mmoja anatambua kama ni
ukombozi katika sekta ya maendeleo.
Waziri Lukuvi alitoa pongezi hizo kwa
Rais Kikwete wakati akiwasalimia wananchi wa jimbo la Isimani ambao
walishiriki hafla fupi ya Rais Kikwete kuweka jiwe
Akitoa taarifa ya ujenzi wa barabara
hiyo waziri wa ujenzi Dkt John Magufuli alisema kuwa wizara yake haitasita
kuwachukulia hatua makandarasi ambao watashindwa kutekeleza mikataba yao kama
ilivyo elekezwa.
Waziri Magufuli alisema kuwa wizara yake
chini ya Rais Kikwete itaendelea kusimamia ujenzi wa barabara na kujenga kwa
kiwango cha lami na kuwa wale wanaopinga jitihada hizo waendelee kusubiri
kuandamana katika barabara zilizojengwa na serikali ya CCM.
Katika hatua nyingine Dkt Magufuli
alimpongeza mbunge wa jimbo la Isiman ,Lukuvi kuwa ni mbunge na waziri mchapa
kazi na kuwa iwapo angekuwa jimboni kwake na kutangaza kugombea ubunge basi
angemwachia jimbo ili agombee.
Waziri Magufuli alisema kuwa ujenzi wa
barabara hiyo ya Iringa -Dodoma yenye urefu wa Km 260 itajengwa kwa zaidi ya
bilioni 232 fedha kutoka benki ya maendeleo Afrika (ADB) na serikali ya Japani
pamoja na serikali ya Tanzania.
Wakati huo huo wafanyakazi na
vibarua wanaofanya kazi katika kampuni hiyo ya kichina
inayotengeneza barabara ya eneo la Migoli katika barabara hiyo ya
Iringa - Dodoma nusuru wavurugu siku baada ya kupaza sauti mbele ya
Rais wakilalamikia fedha kiduchu wanazo pata kwa siku kwa kufanya
kazi katika kampuni hiyo.
Vibarua hao na wafanyakazi
walisikika wakipaza sauti wakati Rais Kikwete akiaga kwa ajili ya
kuelekea katika chakula cha mchana kuwa wanapunjwa sana mishahara na
kuomba kusaidia kupiganiwa ili kulipwa kima cha chini cha mishahara ya
serikali.
"Mheshimiwa Rais una ondoka ila
sisi wafanyakazi tunaomba kusikilizwa kilio chetu ....hawa wachina
wanatufanyisha kazi kwa ujira mdogo sana mheshimiwa tunaomba kusaidiwa
....walipasa sauti wafanyakazi na vibarua hao ambao walikuwa
wamesimama juu ya mashine zao za kazi"
Hata hivyo Rais Kikwete hakuweza
kujibu chochote juu ya madai hayo kutokana na eneo hilo kutawaliwa
na kelele nyingi za burudani na hivyo kushindwa kusikia zaidi ya mkuu
wa mkoa wa Iringa Dkt Christine Ishengoma kuwasikia na kuwajibu kwa
sauti ya chini kuwa ila si mnapata chakula?
0 comments:
Post a Comment