Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Friday, 17 May 2013

Pendekezo la kupewa hifadhi ya ukimbizi Sanogo

 
Serikali ya Benin imetangaza kuwa tayari kumpa hifadhi ya kisiasa Kepteni Amadou Haya Sanogo kiongozi wa wafanya mapinduzi nchini Mali. Nassirou Bako - Arifari Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Benin amesema kuwa, pendekezo la Benin la kumpa hifadhi ya kisiasa Sanogo ni katika juhudi za nchi hizo za kupatikana njia za kurejeshwa demokrasia nchini Mali. Taarifa zinasema kuwa, mauaji, vitendo vya ubakaji, uporaji, utesaji na hata shambulio dhidi ya vituo vya kiutamaduni vya nchi hiyo ni miongoni mwa jinai ambazo zilifanywa katika machafuko yaliyojiri nchini humo, hali ambayo ilisababisha watu wasiopungua laki tatu kuwa wakimbizi. Wakati huohuo, Rais wa mpito wa Mali amesema kuwa, kundi la Tuareg ambalo bado linadhibiti eneo kubwa la kaskazini mwa nchi hiyo ukiwemo mji wa Kidal, limetangaza kuwa tayari kufanya mazungumzo na serikali ya Bamako yenye shabaha ya kukomesha machafuko nchini humo. Rais Douncounda Traore aliyasema hayo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais Francois Hollande wa Ufaransa mjini Paris.

0 comments:

Post a Comment