Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 21 May 2013

'Kundi la LRA la Uganda limefanya mauaji ya halaiki'
 Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa kundi la waasi wa Lord's Resistance Army LRA la nchini Uganda limetekeleza jinai kubwa za kuua maelfu ya watu katika eneo la Afrika Mashariki na ya Kati. Taarifa ya Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa, kundi hilo linaloongozwa na Joseph Kony ambaye anasakwa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC, limewaua zaidi ya watu laki moja katika eneo hilo katika kipindi cha miaka 25 iliyopita. Ban Ki moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, kundi la LRA linatuhumiwa kuwakamata mateka watoto baina ya elfu sitini hadi laki moja na kusababisha pia watu wengine wasiopungua milioni mbili na nusu kuwa wakimbizi. Wakati huohuo, Navi Pillay Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, hivi karibuni itatolewa ripoti ya jinai zilizofanywa na kundi la LRA tokea mwaka 1988. Inafaa kuashiria hapa kuwa, kundi la LRA lilianzisha uasi kaskazini mwa Uganda mwaka 1988, kisha likaelekea na kujizatiti katika maeneo ya mashariki na kaskazini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Sudan Kusini mwaka 2005. 

0 comments:

Post a Comment