15 Rajab,1434
Hijiriyah/ May 25,2013 Miyladiyah
Lambert Mende Omalanga Waziri wa Habari na Msemaji wa serikali ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ametangaza kuwa, Kinshasa iko tayari
kurejea tena kwenye mazungumzo ya amani na kundi la waasi wa M23.
Omalanga ameongeza kuwa, serikali ya Kongo iko tayari kufanya tena
mazungumzo na waasi wa M23 kwa upatanishi wa serikali ya Uganda kwa
shabaha ya kuandaa mazingira ya kuwapokonya silaha kwa njia za amani
wanamgambo wa kundi hilo. Waziri wa Habari wa Kongo amesema kuwa, ujumbe
wa serikali haujawahi kususia mazungumzo hayo, bali ujumbe wa waasi wa
M23 ndio ulioondoka kwenye meza ya mazungumzo ya amani mjini Kampala.
Kwa upande wake, Amani Kabasha Msemaji wa M23 amedai kuwa, tarehe 28
Machi mwaka 2013 serikali ya Kongo ilijiondoa kwenye mazungumzo ya
Kampala, hatua hiyo iliandaa mazingira kwa Baraza la Usalama la Umoja
wa Mataifa kutoa azimio nambari 2098 ambalo lilisababisha kuanza tena
mapigano mashariki mwa nchi hiyo.
Sikiliza Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment