Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday, 16 May 2013

Kiti cha Makueni, Kenya chatangazwa kuwa wazi

                             

 
 
Wiki moja baada ya kuzikwa Seneta wa jimbo la Makueni nchini Kenya, Bw. Mutula Kilonzo, Spika wa bunge la Seneti nchini humo, Ekwe Ethuro ametangaza kiti hicho kuwa wazi; ikiwa na maana kwamba uchaguzi mdogo unaweza kufanyika wakati wowote kujaza nafasi hiyo. Ethuro amesema tayari ameiandikia barua Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC kuhusu uamuzi huo. Tume hiyo sasa inatarajiwa kutangaza tarehe ya kufanyika uchaguzi mdogo huko Makuweni. Mutula Kilonzo alifariki dunia majuma matatu yaliyopita nyumbani kwake na kifo chake kimeendelea kuzusha maswali mengi huku nadharia nyingi zikitolewa kuhusu sababu ya kifo hicho. Timu ya madaktari walioufanyia upasuaji mwili wa Kilonzo kwa ajili ya uchunguzi ilisema matokeo kamili yatatolewa baada ya miezi 2.

0 comments:

Post a Comment