Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday 2 May 2013

"Kenya itaendelea kulinda uhuru wa wanahabari

                       23Jumaadal Aakhir,1434 Hijiriyah/ May 03,2013 Miyladiyah

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ameahidi kuwa, serikali yake itaendelea kuheshimu na kulinda uhuru wa wanahabari pamoja na vyombo vya habari nchini humo. Akizungumza leo wakati wa kufungua rasmi mkutano wa kimataifa wa waandishi wa habari mjini Nairobi, Rais Kenyatta amesema sekta ya uandishi habari ni kiungo muhimu katika jamii na kwa mantiki hiyo amevitaka vyombo vya habari kuwajibika zaidi kwa manufaa ya Wakenya. Rais wa Kenya aidha ameonya vyombo vya habari ambavyo hutumiwa na wanasiasa kuchochea fujo na machafuko kwamba serikali yake haitasita kuvichukulia hatua kali za kisheria. Ametoa mfano wa mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994 ambayo yalichochewa zaidi na vyombo vya habari na kusema serikali haitowavumilia wenye nia ya kuivuruga nchi. Mkutano huo wa kimataifa unawashirikisha wanahabari kutoka nchi mbalimbali duniani na unatarajiwa kumalizika hapo kesho wakati dunia itakuwa inaadhimisha siku ya kimataifa ya kutetea uhuru wa wanahabari.

0 comments:

Post a Comment