Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday 16 May 2013

Jukwaa la Katiba TZ kuishtaki tume ya Warioba

                           

 
Mwenyekiti wa jukwaa la katiba nchini Tanzania, Deus Kibanda  amesema asasi yake  inapanga kuwasilisha kesi  mahakamani  kuzuia mchakato wa katiba mpya kutokana na mapungufu ambayo tume ya katiba nchini humo imedaiwa kuyafumbia macho. Kibanda amefafanua kuwa, miongoni mwa mapungufu yaliyopewa kisogo na Tume ya Mabadiliko ya Katiba inayoongozwa na Jaji mustaafu, Joseph Warioba ni pamoja na vyama vya siasa kuteka nyara mchakato wa mabadiliko ya katiba, wananchi kukosa kuelimishwa barabara kuhusu mchakato huo na kukosa kuhusishwa kikamilifu wadau wa shughuli hiyo ya kuunda katiba mpya. Hii ni katika hali ambayo, Chama cha upinzani cha CUF kimesema kupitia mwenyekiti wake Profesa Ibrahim Haruna Lipumba kwamba, serikali inapanga mkakati wa kuvuruga mchakato wa kuandaa rasimu ya katiba mpya ili iweze kubakia madarakani kwa zaidi ya muda wa miaka 5 ulioainishwa na katiba ya sasa.

0 comments:

Post a Comment