Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 21 May 2013

Ban atiwa wasi wasi na matukio Madagascar

Ban Ki-moonKatibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ameonyesha wasiwasi wake kuhusiana na mwenendo wa uchaguzi ujao nchini Madagascar. Ban amesema hayo leo na kuongeza kuwa, Umoja wa Afrika AU na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa pamoja zina wasiwasi kuhusiana na hali ya Madagascar kuelekea uchaguzi ujao wa rais na kuitaka mirengo yote ya kisiasa nchini humo kufanya juhudi za haraka za kuafikiana juu ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa, UN inaunga mkono mabadiliko nchini humo na kuyataka makundi ya kisiasa kukaa kwenye meza moja ya mazungumzo. Aidha ameyataka makundi ya kisiasa kufumbia macho baadhi ya matakwa yao ya kisiasa ili kuiepusha serikali ya mpito iliyoko madarakani na matatizo makubwa zaidi. Matamshi hayo yametolewa katika hali ambayo, siku ya Ijumaa Umoja wa Afrika ulitangaza kuwa, hautamtambua Andry Rajoelina Rais wa mpito wa Madagascar iwapo atachaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo, kwenye uchaguzi ujao.

0 comments:

Post a Comment