Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Saturday, 18 May 2013

AU kutomtambua Rajoelina uchaguzi Madagascar

Umoja wa Afrika umesema kuwa, hautamtambua Andry Rajoelina Rais wa mpito wa Madagascar iwapo atachaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo, kwenye uchaguzi ujao wa rais. Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika limetangaza kuwa, wale wote waliosababisha serikali na katiba kubadilishwa nchini humo wanazuiliwa kushiriki kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi huo. Baraza hilo limesema kuwa, Rajoelina aliingia madarakani mwaka 2009, baada ya kuuangusha utawala halali wa Rais Marc Ravalomanana kiongozi wa zamani wa nchi hiyo. Hivi karibuni Umoja wa Ulaya ulitangaza kutowatambua viongozi wa Madagascar ambao watachaguliwa kinyume na maagizo ya Umoja wa Afrika au Jumuiya ya Ustawi ya Kusini mwa Afrika SADC, ambayo ndio mpatanishi wa mgogoro wa Madagasca

0 comments:

Post a Comment