Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday 28 May 2013

Al Bashir atishia kuizuwilia mafuta Juba

Vikosi vya serikali ya Sudan vimepigana na waasi wa Kordofan kusini.Rais Omar Hassan al Bashir ameionya serikali ya Juba,nchi yake itayafunga mabomba ya mafuta ikiwa Sudan Kusini itaendelea kuwaunga mkono waasi.
Wakimbizi wa Kordofan kusini waliokimbia mapigano katika mji wa Kadugli mwaka 2011
Mapigano hayo yaliripuka jumapili iliyopita katika eneo la Dandor,umbali wa kilomita 500 magharibi ya mji mkuu wa Sudan-Khartoum.
Msemaji wa jeshi la Sudan,kanali Sawarmy Khaled amesema vikosi vya serikali vimepigana na waasi walioushambulia mji wa Dondor na kuwauwa zaidi ya 70 pamoja na kuviteka vifaru vyao viwili.Taarifa ya kanali Khaled iliyotangazwa na kituo rasmi cha matangazo-.Radio Omdurman,haikusema hasara iliyopatikana upande wa vikosi vya serikali.
Hata hivyo,waasi kupitia msemaji wa jeshi la ukombozi wa watu wa kaskazini SPLA-N,Arnu Ngutullu Loddi amesema vikosi vya serikali vimepata hasara kubwa kutokana na mapigano hayo.
Hakuna habari huru zinazothibitisha madai ya upande wowote ule.
Wasai wameonya mapigano zaidi yataripuka dhidi ya vikosi vya serikali ya Sudan na wanamgambo wanaowaunga mkono.
Wengi kati ya wakaazi milioni moja na laki noja wa Kordofan Kusini wanasemekana kuelemea zaidi upande wa Sudan kusini na wanaishi katika eneo linalodhibitiwa na SPLA-N
Serikali ya mjini Khartoum kila kwa mara imekuwa ikiishutumu serikali ya Juba kuwaunga mkono waasi-madai yanayokanushwa kila wakati na Sudan kusini.
Al Basahir atishia kufunga mabomba ya mafuta
 
Marais Omar al-Baschir wa Sudan na Salva Kiir wa Sudan Kusini

Rais Omar al Bashir wa Sudan ameonya atayafunga mabomba yanayoipatia mafuta Sudan kusini ikiwa Juba haitaacha kuwaunga mkono waasi.
Onyo hilo amelitoa katika hafla ya kusherehekea kukombolewa na jeshi la Sudan mji wa Abou Kershola toka mikononi mwa waasi wa Kordofan kusini.
 

0 comments:

Post a Comment