Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday, 23 May 2013

Aina hatari ya Polio yasambaa Kenya na Somalia

Shirika la Afya Duniani WHO linasema eneo la Pembe ya Afrika limekumbwa na aina mpya na hatari ya ugonjwa wa polio kwa kifupi WPV1. Mtoto wa umri wa miezi minne aliripotiwa kuonekana akiwa na dalili za ugonjwa huo na kulemaa karibu na kambi ya Dadaab nchini Kenya mnamo tarehe 30 mwezi Aprili mwaka huu.
Utafiti kuhusu ugonjwa huu unaendelea. Ili kukabiliana na mkurupuko huo kampeni ya kwanza ya utoaji wa chanjo ikiwalenga watoto 440,000 ilianza mwezi Mei mwaka huu nchini Somalia huku awamu ya pili ikipangwa kuanza tarehe 26 mwezi huu kwenye sehemu zilizoathirika nchini Kenya. WHO imesema hatari kwa mataifa jirani ni ya juu kutokana na kuhama hama kwa watu wengi kwenye Pembe Ya Afrika. Kambi ya Dadaab iliyoko kaskazini mashariki mwa Kenya ni makao ya karibu wakimbizi 500,000 kutoka sehemu tofauti za Pembe ya Afrika. Tahadhari ya kutaka ufanyike utafiti imetolewa kwa nchi zote katika Pembe ya Afrika ya kutaka vifanyiwe uchunguzi visa vyote. Mwaka 2005 ugonjwa wa polio ulisambaa kutoka barani Afrika hadi nchini Yemen ambapo visa 700 vya ugonjwa huo viliripotiwa. Tangu wakati huo chanjo mpya za ugonjwa wa polio zimebuniwa ambazo zitazuia mikurupuko ya ugonjwa wa polio kwa muda mrefu.

0 comments:

Post a Comment