Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 28 May 2013

176 wauliwa na kujeruhiwa kwenye milipuko 21 Iraq
Watu wasiopungua 176 wameuawa na kujeruhiwa baada ya kujiri milipuko 21 ambapo 17 kati ya hiyo ilikuwa ya utegaji mabomu ndani ya magari kwenye maeneo mbalimbali huko Baghdad mji mkuu wa Iraq. Taarifa zinasema kuwa, watu wasiopungua 85 wameuawa na wengine wasiopungua 90 kujeruhiwa kwenye milipuko hiyo iliyotokea ndani ya muda wa masaa mawili tu mjini Baghdad. Milipuko hiyo imetokea katika hali ambayo, majeshi ya ardhini na angani ya nchi hiyo siku ya Jumapili yalitekeleza oparesheni kubwa  katika mikoa ya al Anbar ulioko magharibi, Babil ulioko katikati,  Karkuk ulioko kaskazini  na mkoa wa Diyala ulioko mashariki mwa Iraq na kufanikiwa kuwaangamiza magaidi 14 na kuwakamata wengine 76.

0 comments:

Post a Comment