Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 21 May 2013

10 wafungwa jela kwa kutetea hijabu Azerbaijan Watu wasiopungua 10 wamehukumiwa adhabu ya kifungo cha kati ya miezi 18 hadi 24 jela nchini Jamhuri ya Azerbaijan baada ya kupatikana na hatia ya kulalamikia marufuku ya uvaaji wa hijabu kwenye shule za nchi hiyo. Mahakama ya Baku imetoa hukumu hiyo kwa watu hao waliokuwa wakipinga marufuku iliyowekwa na serikali ya kuvaa hijabu mashuleni. Inafaa kuashiria hapa kuwa, kundi la wananchi  lilifanya maandamano makubwa mwezi Oktoba mwaka jana mbele ya Wizara ya Elimu ya Azerbaijan, likilalamikia marufuku ya uvaaji hijabu mashuleni na kusababisha watu kadhaa kutiwa mbaroni baada ya askari polisi kupambana na waandamanaji hao waliokuwa na hasira. Inafaa kuashiria hapa kuwa asilimia 99.2 ya wananchi wa Jamhuri ya Azerbaijan ni wafuasi wa dini ya Kiislamu.

0 comments:

Post a Comment