Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday 23 April 2013

ZIARA YA MAKAMU MWENYEKITI WA CCM ZANZIBAR



 MAKAMO Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dkt Ali Muhammed Shein awataka viongozi wa chama cha mapinduzi kudumisha na kuimarisha nguvu zao za chama kwa kufuata sera ilani na maadili ya chama hicho .
Alisema kila kiongozi inampasa atumikie chama kwa misingi iliyowekwa na kuzingatia mashirikiano na umoja uliopo katika chama .
Aliyasema leo huko Amani Ofisi ya CCM Mkoa wa Mjini alipokuwa akitoa majumuisho ya ziara yake ya wilaya ya mjini katika mfululizo wa ziara za kutembelea mikoa na wilaya za chama Zanzibar .
soma zaidi

"sisi tukipunguza kasi na wenzetu wanaengeza kasi lazima tubadilike sote tulipata tabu sana wakati wa uchaguzi ".Alisema Makamo Mwenyekiti wa CCM.
Aidha alisema kuwa lengo kuu la ziara hiyo ni kuweza kujua maendeleo changamoto pamoja na matatizo mbali mbali yanayojitokeza katika mikoa na wilaya ya Zanzibar.
Sambamba na hayo Dkt Shein alisema kuwa anaelewa kwamba vijana wengi wanaka biliwa na tatizo la ajira hivyo aliwataka vijana hao hujikusanya kwa makundi ili kuweza kupata mikopo ya kujikimu na maisha na kupunguza umasikini .
Alieleza kuwa Serikali imeweka Wizara ya Kazi Uwezeshaji Kiuchumi na Ushirika kwa lengo la kuwasaidia wananchi mbali mbali kwa kuwapatia mikopo nafuu ili kuepukana na ukali wa maisha .
Alisema kuwa pesa zipo na nyingi sana ambazo bado hazijatolewa za mfuko wa miradi ya maendeleo kwa wananchi, mfuko ambao ulianzishwa na Mhe Ali Hasan Mwinyi Rais wa Jamhuri wa Muungano Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Rais Mstaafu Amani Abeid Karume pamoja na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Alifahamisha kuwa kuna pesa nyingi ambazo zimekopwa katika Benki ya Dunia kwa ajili ya kuendeleza mradi wa kuimarisha huduma za Mji Mkongwe wa Zanzibar ambao kwa sasa hauridhishi ni mchafu mno .
Alisema kuwa kupitia pesa hizo kutaimarishwa kwa kutiwa taa za solar za kutumia jua, vyombo mbali mbali vya usafi pamoja na kutengwa sehemu maalum ya kutupia taka.
.
Nao wanachama wa CCM walipata nafasi ya kuelezea matatizo yao walisema kuwa kuna baadhi ya watu wamejitokeza kutishia maisha ya watu na mali zao jambo ambalo litasababisha kupoteza amani katika nchi .
Pia walisema sababu zinazopelekea chama kuzoroteka kunatokana na Viongozi wa juu kutokuwa na mashirikiano na umoja katika kukiimarisha Chama cha Mapinduzi.
Hata hivyo wanachama hao wamemuomba Makamo Mwenyekiti kuwafikiria wastaafu kwa kuwaongezea pencheni zao .
IMETOLAWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

0 comments:

Post a Comment