Naibu Rais wa Kenya, William Ruto amesema takriban watu 63 wamefariki
dunia na zaidi ya 35 000 wameachwa bila makao kufuatia mafuriko
yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo
mbalimbali ya nchi hiyo. William Ruto amesema serikali inafanya juu
chini kuona walioathirika wanapata misaada haraka iwezekanavyo. Naibu
rais pia ameliamuru jeshi lisaidie kufanikisha zoezi la kuwaondoa watu
katika maeneo yanayoendelea kushuhudia mvua kubwa na ambayo huenda
yakakumbwa na mafuriko siku chache zijazo. Ruto pia ametaka shirika la
Msalaba Mwekundu kuchukua hatua za haraka ili kuwasaidia watu waliofikwa
na janga hilo la kimaumbile. Idara ya hali ya hewa imetahadharisha kuwa
maeneo mengine mengi ya Kenya huenda yakakumbwa na mafuriko kwani mvua
zitaendelea kunyesha. Hadi sasa maeneo ya kaskazini mashariki na baadhi
ya maeneo ya Pwani nchini humo ndiyo yaliyoathiriwa pakubwa na mafuriko
hayo.
Sikiliza Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment