Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 9 April 2013

Uhuru Kenyatta kuapishwa leo KenyaViongozi na wakuu wa nchi 25 watahudhuria sherehe za kuapishwa  Uhuru Muigai  Kenyatta, Rais mpya wa Kenya zilizopangwa kufanyika leo mjini Nairobi.

Taarifa zinasema kuwa, Marais Jacob Zuma wa Afrika Kusini, Yoweri Museveni wa Uganda, Jakaya Kikwete wa Tanzania, Michael Sata wa Zambia, Ismail Guelleh wa Djibouti, Salva Kiir wa Sudan Kusini na Hailemariam Desalegn Waziri Mkuu wa Ethiopia tayari wameshawasili nchini Kenya.

Uhuru Kenyatta mwenye umri wa miaka 51 kutoka mrengo wa Jubilee alishinda uchaguzi wa rais uliofanyika Machi 4 kwa kupata asilimia 50.7 ya kura na kumbwaga mpinzani wake Raila Odinga aliyepatia asilimia 43.3 ya kura zote.
Uhuru anachukua uongozi wa nchi hiyo akiwa ni rais wa nne tokea nchi hiyo ilipojipatia uhuru kutoka kwa mkoloni Muingereza. Rais wa kwanza wa Kenya ni baba yake mzazi  Mzee Jomo Kenyatta aliyeongoza kuanzia mwaka 1964 hadi 1978, akafuata Daniel Arap Moi, na baadaye akaja Mwai Kibaki. Katika sherehe za leo pia, ataapishwa William Ruto ambaye ataku0 comments:

Post a Comment