Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Saturday, 13 April 2013

‘Sudan mbili zitarejesha uhusiano wao wa kawaida’

Rais Omar al Bashir wa Sudan amesema uhusiano wa nchi yake na Sudan Kusini utarejea katika hali ya kawaida na kuanzishwa pia ushrikiano wa mpakani kati ya nchi mbili. Al Bashir ameyasema hayo katika hotuba aliyotoa hapo jana huko Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini akiwa katika safari yake ya kwanza huko tangu Julai mwaka 2011 wakati eneo la kusini mwa Sudan lilipojitenga na nchi hiyo na kuwa taifa huru la Sudan Kusini. “Ziara hii inaonyesha mwanzo wa ushirikiano wenye lengo la kurejesha uhusiano katika hali ya kawaida baina ya nchi mbili”, amesema Rais wa Sudan. Kwa upande wake Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amesema amekubaliana na mwenzake wa Sudan kuendeleza mazungumzo ili kutatua masuala yote yenye mzozo kati ya majirani hao wawili. Amesema baadhi ya masuala yanahitajia majadiliano zaidi na kuongeza kuwa amekubali mwaliko aliopewa na al Bashir wa kuitembelea Sudan hivi karibuni ambayo itakuwa safari yake ya pili nchini humo tangu kusini mwa Sudan ilipojitenga na Sudan. Mataifa hayo mawili yalikubaliana mwezi Machi kuanzisha tena usafrishaji wa mafuta ya Sudan Kusini kupitia mpaka wa Sudan na kuchukua hatua za kupunguza mvutano baina yao. Hata hivyo nchi hizo mbili bado hazijafikia makubaliano juu ya nani ana haki ya kumiliki mkoa wa Abyei pamoja na maeneo mengine yanayozozaniwa katika eneo la mpaka wa pamoja wenye urefu wa kilomita 2,000…/

0 comments:

Post a Comment