Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday 16 April 2013

Sudan kuipeleka Uganda mahakama ya kimataifa


                                                        06Jumaadal Aakhir,1434 Hijiriyah/ April 16,2013 Miyladiyah
Serikali ya Sudan ina azma ya kuifungulia mashtaka serikali ya Uganda kwenye mahakama ya kimataifa kutokana na hatua ya nchi hiyo ya kuyaunga mkono makundi ya waasi wa Sudan.
Ibrahim Ghandour mkuu wa timu ya mazungumzo kati ya Sudan na Sudan Kusini amesema kuwa, Uganda imefanya njama kadhaa dhidi ya Sudan na kwa minajili hiyo serikali ya Khartoum imefikia uamuzi wa kuifungulia mashtaka serikali ya Kampala, ili iache kuwaunga mkono waasi wa Sudan. Ameongeza kuwa, Uganda licha ya kuwaunga mkono waasi hao inawapatia hifadhi ndani ya ardhi ya nchi hiyo.
Inadaiwa kuwa, makundi ya waasi wa Sudan yamekuwa yakipata uungaji mkono wa madola ya kigeni kama vile Sudan Kusini na Uganda ili kusababisha machafuko katika majimbo ya Blue Nile na Kordofan Kusini.

0 comments:

Post a Comment