Serikali mpya ya wafanyamapinduzi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati,
imetangaza kuwa, imenasa aina kadhaa za silaha zilizokuwa zimedhibitiwa
na wafuasi wa Rais wa zamani wa nchi hiyo Francosi Bozize. Waziri wa
Mawasiliano wa serikali mpya ya Jamhuri ya Afrika ya Kati Christophe
Gazam Betty ametangaza kuwa, silaha hizo zimenaswa katika eneo la Boy
Rabe katika viunga vya mji mkuu Bangui. Aidha waziri huyo wa mpito
amesema kuwa, mbali na silaha hizo zilizonaswa, askari wa Seleka pia
wamewatia mbaroni askari wa gadi ya rais aliyepinduliwa madarakani
nchini humo Francois Bozize ambaye hivi sasa anaishi uhamishoni nchini
Benin. Gazam Betty ameongeza kuwa, askari wa Seleka wanaendelea na
oparesheni kali ya kusaka silaha zinazodhibitiwa na wafuasi wa rais huyo
wa zamani wa CAR. Hii ni katika hali ambayo hivi karibuni mamia ya
wananchi wa nchi hiyo walifanya maandamano dhidi ya muungano wa waasi wa
Seleka uliotwaa madaraka mwezi uliopita baada ya kuiangusha serikali ya
Rais Francois Bozize.
Sikiliza Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment