Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 23 April 2013

Serikali iharakishe sheria ya fidia kazini

                  

 
MBUNGE wa Viti Maalumu, Amina Makilagi (CCM) ameitaka serikali kuharakisha sheria ya kuwalipa fidia watu wanaopata maumivu na ulemavu wakiwa kazini.
Makilagi alitoa kauli hiyo bungeni jana alipouliza swali la nyongeza na kutaka kuelewa ni kwanini serikali imechelewesha kuleta sheria hiyo bungeni wakati muswada ulipitishwa tangu mwaka 2008.
Katika swali la msingi, mbunge huyo alitaka kujua serikali imefikia hatua gani katika kufanya ukaguzi wa afya na usalama mahali pa kazi, ili kuimarisha utendaji katika maeneo yao ya kazi.
Akijibu swali hilo, Naibu wa Wizara ya Kazi na Ajira, Makongoro Mahanga, alikiri kuwa sheria hiyo imechelewa kutokana na ufinyu wa bajeti ya wizara kwa ajili ya kutengeneza kanuni.
Aidha, alisema kutokana na ufinyu wa fedha bado Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) hawana uwezo mkubwa wa kufanya kazi zao.
Makongoro alieleza kuwa katika mwaka wa fedha 2011/12 OSHA ilifanya ukaguzi wa ndani ambao ni wa kawaida, ambapo ni sawa na asilimia 85 ya ukaguzi uliopangwa.

0 comments:

Post a Comment