Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday 9 April 2013

NMB yasaidia madawati shule ya Ruvu

 
BAADHI YA WAFANYAKAZI WA BENKI YA NMB KUTOKA MAKAO MAKUU, KUTOKA KULIA NI JEREMIAH LYIMO,DICKSON PANGAMAWE,BORONDO CHACHA NA BEATRICE MWAMBIJE.
 
 
BENKI ya NMB tawi la Kibaha imetoa msaada wa madawati 65 kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Ruvu Stesheni ili kuwasaidia waweze kusoma katika mazingira mazuri.
Akikabidhi madawati hayo katika sherehe fupi iliyofanyika shuleni hapo, Ofisa Tawala wa NMB Kanda ya Mashariki, Lilian Abraham alisema msaada huo umegharimu sh milioni 5.
Lilian alisema NMB imeamua kujikita kusaidia sekta ya elimu ili kuleta mabadiliko chanya kwa wanafunzi waweze kujisomea kwa bidii na kuweza kuongeza kiwango cha ufaulu.
“Sisi kwa kweli lengo letu kubwa ni kuhakikisha tunakuwa mstari wa mbele katika kusaidia maendeleo ya elimu, kwani tunatambua kuna changamoto nyingi zilizopo katika baadhi ya shule, lakini kwa hiki kidogo ambacho tumekitoa leo nina hakika kitaweza kuwasaidia  kwa kiwango kikubwa watoto wetu,” alisema.
Ofisa Elimu wa Wilaya ya Kibaha, Winfrida Mbuya ambaye alipokea msaada huo kwa niaba ya shule, alimshukuru Mbunge wa Kibaha Vijijini, Abuu Jumaa kwa kuomba msaada huo NMB na kuwataka wadau na wahisani mbalimbali kujitokeza kwa wingi kusaidia kuchangia  sekta ya elimu.
Meneja NMB tawi la  Kibaha, Hassan Mpangachuma, alisema wataendelea kutoa misaada mingine kwa kutambua umuhimu mkubwa uliopo katika sekta ya elimu na changamoto zinazowakabili wanafunzi.
Akishukuru kwa niaba ya walimu wenzake, Mkuu wa shule hiyo, Shaban Rajabu alisema msaada huo ni mkombozi mkubwa kwa upande wao, japo bado wanakabiliwa na uhaba wa meza, viti pamoja na vitabu.

0 comments:

Post a Comment