Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Friday, 19 April 2013

Nchi za Afrika zaafiki kupelekwa wanajeshi CAR

                  10Jumaadal Aakhir,1434 Hijiriyah/ April 20,2013 Miyladiyah
Marais wa nchi zilizoko katika eneo la katikati mwa bara la Afrika wameafiki kwa kauli moja mpango wa kupelekwa wanajeshi 2,000 katika Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa shabaha ya kurejesha amani na uthabiti nchini humo. Kwenye kikao cha dharura kilichofanyika jana nchini Chad, wakuu hao wamesisitiza juu ya kutumwa kikosi cha dhiba kitakachotekeleza operesheni ya kukomesha machafuko na uporaji wa mali katika miji mbalimbali ya nchi hiyo. Aidha wakuu wa nchi za eneo la katikati mwa bara la Afrika wameeleza kuwa, rais, waziri mkuu, mawaziri wa serikali ya mpito na hali kadhalika wajumbe wa Baraza la Taifa la Mpito hawataruhusiwa kugombea nafasi yoyote kwenye uchaguzi ujao. Taarifa ya wakuu hao imeeleza kuwa, uchaguzi mkuu ujao unapaswa kuwa huru na wa haki, utakaofanyika katika kipindi cha miezi 18 kuanzia sasa, ili kurejesha utawala na mfumo wa katiba nchini humo.

0 comments:

Post a Comment