Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday, 11 April 2013

‘Mwinyi yuko sahihi kuhusu kuchinja’

SHEIKH wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, amesema kauli ya Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, kuhusu kila mtu ruksa kuchinja iko sawa.
Akizungumza  jana jijini Dar es Salaam jana, Alhad Mussa, alisema Mwinyi hajakosea kutoa kauli hiyo, bali alichosema ni kwamba kila mtu anaweza kuchinja kutokana na imani yake ili mradi havunji sheria ya nchi.
Alisema kusudio la kauli ile ilikuwa ni kuwafahamisha wananchi kwamba Wakristo wanaweza kuchinja kitoweo chao na wakala endapo wako katika familia zao.
Hata hivyo, alisema kutokana na ustaarabu uliojengeka tangu awali Waislamu wataendelea kuchinja kitoweo cha jamii yote kama ilivyokubaliwa na maaskofu na masheikh.
Alisema hali hiyo haina maana kwamba Waislamu ni bora kuliko watu wa dini nyingine, bali inatokana na miiko ya dini yao ya kutokula kitoweo kilichochinjwa na dini nyingine.
“Unajua wenzetu hawana miiko, dini yao inawaruhusu kula kitoweo kilichochinjwa na Waislamu na ndiyo maana wako tayari hata kuchinjiwa kitoweo chao na Waislamu,” alisema.
 

0 comments:

Post a Comment