Rais Gabriel Robert Mugabe wa Zimbabwe amesema hatoruhusu wageni
kuingilia zoezi la uchaguzi mkuu ujao na badala yake amewataka
Wamagharibi kuheshimu uhuru wa kujitawala wa nchi yake. Akizungumza leo
Alhamisi wakati wa kuadhimisha miaka 33 ya uhuru wa Zimbabwe, Rais
Mugabe amesema nchi ambazo zimefungua milango kwa Wamagharibi
kujipenyeza zimeendelea kubaki nyuma kimaendeleo. Kiongozi huyo ametoa
wito kwa Wazimbabwe kujitokeza kwa wingi wakati wa uchaguzi mkuu
unaotarajiwa kufanyika kati ya mwezi Juni na Septemba mwaka huu. Pia
amesema wananchi wako huru kumchagua kiongozi yeyote wampendaye.
Amewahakikishia Wazimbabwe kwamba uchaguzi huo utakuwa huru na wa haki.
Inafaa kukumbusha hapa kuwa uchaguzi mkuu ujao nchini Zimbabwe utakuwa
wa kwanza chini ya katiba mpya na utaashiria mwisho wa serikali ya umoja
wa kitaifa iliobuniwa mwaka 2009 ambapo Rais Mugabe alilazimika
kugawana madaraka na hasimu wake wa muda mrefu, Morgan Tsvangirai.
Sikiliza Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment