Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 9 April 2013

Mkuu wa Tume ya Maulamaa Somalia anusurika kifo

Mkuu wa jopo la Maualaa nchini Somalia, ameponea chupuchupu kuuawa katika mripuko uliotokea leo mjini Mogadishu. Sheikh Bashir Ahmed Salad ameokoka na kifo licha ya kutokea mripuko ndani ya gari yake katika eneo la Hodan, kusini mwa mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, bali hata hakujeruhiwa katika mripuko huo. Hadi sasa hakuna kundi lolote lililotangaza kuhusika na shambulio hilo ingawa kundi la ash Shabab linadhaniwa kuhusika na shambulio hilo. Kundi la ash Shabab ambalo bado linadhibiti baadhi ya maeneo ya katikati na kusini mwa Somalia, kwa mara kadhaa limekuwa likifanya mashambulizi dhidi ya vikosi vya serikali na vile vya Umoja wa Afrika AMISOM katika mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu.

0 comments:

Post a Comment