Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 23 April 2013

Mgomo wakwamisha safari za ndege Ujerumani


Shirika la ndege la Lufthansa linalomilikiwa na serikali ya Ujerumani limelazimika kufutilia mbali safari za ndani ya nchi, zile za bara Ulaya na hata za kimataifa kutokana na mgomo wa wafanyakazi wake wakiwemo marubani.
Lufthansa ambalo ni miongoni mwa mashirika makubwa ya usafiri wa ndege duniani linakabiliwa na matatizo makubwa ya fedha na wafanyakazi wameamua kugoma ili kuishinikiza serikali kuboresha mazingira yao ya kazi pamoja na kuongezwa mishahara yao.
Wataalamu wa masuala ya uchumi wanasema mgomo huo ulioanza leo utaisababishia Ujerumani hasara ya mamilioni ya dola na hivyo kuyumbisha zaidi uchumi wa Ulaya.
Mazungumzo kati ya wafanyakazi wa shirika hilo na serikali kuhusu nyongeza ya mishahara yamefanyika katika duru tatu na kumalizika bila ya makubaliano yoyote

0 comments:

Post a Comment