Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Saturday 13 April 2013

Mbunge ataka kilimo cha bangi kihalalishwe

MBUNGE wa Nkasi, Ally Kessy (CCM) ametoa mpya bungeni baada ya kuuliza swali la kuitaka serikali ihalalishe kilimo cha bangi ili kujipatia fedha za kigeni.
Akiuliza swali la nyongeza jana, Kessy alisema kwa kuwa zao la tumbaku limekuwa likipigwa marufuku dunia nzima, lakini limendelea kulimwa na kuchangia pato la mataifa mbalimbali ikiwemo Tanzania, kwanini serikali isihalalishe kilimo cha bangi kama ilivyo kwa tumbaku ili kuchangia pato la taifa?
Swali hilo liliibua vicheko kwa wabunge wote, akiwemo Spika na Naibu Waziri wa Kilimo na Chakula, Adam Malima.
Hata hivyo, Waziri Malima akijibu swali hilo alisema kuwa pingamizi dhidi ya zao la tumbaku duniani limepungua na zao hilo sasa ni moja ya mazao makubwa ya biashara.
Kuhusu bangi kuhalalishwa kuwa zao la biashara, Waziri Malima alisema kuwa katika nchi zingine imeruhusiwa kuwa moja ya zao la biashara na linachangia pato la taifa.
“Hapa nchini bado bangi haijaruhusiwa kuwa zao la biashara, lakini kama utafiti utafanyika na kubaini kama linaweza kupata soko la kuingizia pato taifa, tutaliangalia hilo,” alisema.
 

0 comments:

Post a Comment