Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 9 April 2013

Mazungumzo ya serikali ya Kongo na M23 yaanza


Msemaji wa kundi la waasi wa M23 ametangaza kuwa mazungumzo ya amani kati ya kundi hilo na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yameanza katika mji mkuu wa Uganda, Kampala.
Duru za habari kutoka Kampala zimearifu kuwa, Rene Abandi anaongoza ujumbe wa waasi wa M23 kwenye mazungumzo hayo na kwamba pande mbili zimekutana na mpatanishi wa Uganda katika vikao tofauti.
Mazungumzo hayo yalianza Disemba mwaka uliopita chini ya usimamizi wa taasisi ya eneo la Ukanda wa Maziwa Makuu ya Afrika lakini yalisimama mwishoni mwa mwezi Februari kutokana na sababu mbalimbali.
Harakati ya M23 inahesabiwa kuwa kundi kubwa zaidi la waasi huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na mwaka uliopita lilizusha mgogoro mkubwa na mapigano kwenye eneo hilo.0 comments:

Post a Comment