Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Wednesday 24 April 2013

Mazungumzo ya amani yaanza Sudan





Umoja wa Afrika (AU) kwa mara ya kwanza umeikutanisha Sudan na makundi ya waasi yanayopigana dhidi ya serikali katika majimbo mawili ya mpakani mwa Sudan Kusini kwa ajili ya mazungumzo ya amani.
Ujumbe wa AU ukiongozwa na Thabo Mbeki rais wa zamani wa Afrika Kusini ulikutana na Ibrahim Ghandour mwakilishi wa serikali ya Sudan na Yassir Arman kiongozi wa wasi wa SPLM- kaskazini mjini Addis Ababa, mwanzoni mwa mazungumzo hayo. Wawakilishi hao wamekubaliana kukutana tena hapo baadaye.
Mapigano kati ya jeshi la Sudan na waasi wa Sudan People's Liberation Movement tawi la kaskazini, yalianza katika jimbo la Kordofan Kusini na Blue Nile baada ya Sudan Kusini kujitenga na Sudan mwaka 2011. Machafuko hayo yamewaathiri karibu watu laki 9 na kuwalazimisha watu wengi kukimbia makazi yao.

0 comments:

Post a Comment