Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 9 April 2013

Lipumba awashauri watu wa Tanga kufufua uchumi


Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amewataka wakazi wa Mkoa wa Tanga, kushikamana ili kufufua uchumi wao, nyinginevyo mkoa huo unaweza kuwa wa mwisho katika ukusanyaji wa pato la taifa.
Pamoja na kuwa na bandari na reli, mkoa huo una fursa nyingi za kuwezesha kuchangis kwa kiwango kikubwa katika pato la taifa.
Akizungumza katika kongamano la kufufua uchumi wa Mkoa wa Tanga juzi, Profesa Lipumba alisema wenyeji wa mkoa huo ndio wenye dhamana na jukumu la kusimamia maendeleo yao.
Alisema bandari na viwanda kadhaa vilivyoko mkoani humo, ni sehemu ya rasilimali za kuiwezesha Tanga kupiga hatua za kimaendeleo na hasa katika uchumi.
“Lakini pia kuongeza ajira kwa vijana wa ndani na nje ya mkoa huo, kwa hiyo watu wa Tanga lazima mshikamane kama mnataka kupiga hatua za kiuchumi,” alisisitiza.
Lipumba alisema Mkoa wa Tanga kwa nyuma kimaendeleo kunatokana na viongozi wake walioko Serikalini, kuendeleza ubinafsi na kuacha kuzitumia nafasi zao kupigania maendeleo.
Akizungumza katika kongamano hilo, Mbunge wa Bunge la Afrika ya Mashariki, Twaha Issa Taslima, alisema Mkoa wa Tanga unaweza kupiga hatua kibiashara ikiwa tu utazitumia fursa zilizopo hasa baada ya kufunguliwa kwa Soko la Pamoja la Afrika ya Mashariki.
Aliwataka wafanyabiashara kulitumia soko hilo kwa uwezo wao wote kwa kuzingatia kuwa litawawezesha kupiga hatua kubwa za kimaendeleo.    

0 comments:

Post a Comment