Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday, 11 April 2013

Kikwete mgeni rasmi siku ya Muungano

02Jumaadal Aakhir,1434 Hijiriyah/ April 12,2013 Miyladiyah
RAIS Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za maadhimisho ya miaka 49 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zitakazofanyika Aprili 26, mwaka huu katika viwanja vya Uhuru jijini Dar es Salaam.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Idara ya Habari (Maelezo), ilieleza sherehe hizo itakazoanza saa 1:00 asubuhi, zitahudhuriwa na viongozi maarufu mbalimbali wakiwamo viongozi waaandamizi wa Tanzania Bara na Zanzibar.
Taarifa hiyo ilieleza kaulimbiu ya sherehe hizo ni ‘Amani, Utulivu na Maendeleo ni matokeo ya Muungano wetu, tuuenzi na kuulinda.’
Maadhimisho hayo ni kumbukumbu ya Muungano uliozaliwa Aprili 26, mwaka 1964 ambapo Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, aliyekuwa rais wa Tanganyika aliungana na Zanzibar chini ya uongozi wa Abeid Aman Karume.

0 comments:

Post a Comment