Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Tuesday, 9 April 2013

Kagame: Waliofanya mauaji ya kimbari wakamatwe
Rais Poul Kagame wa Rwanda amezitaka nchi kadhaa duniani kuwatia mbaroni washukiwa wa mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994.

Rais Kagame amesisitiza kuwa, mataifa yote duniani yanapaswa kufanya juhudi za kuwatia mbaroni washukiwa wote wa mauaji ya kimbari yaliyofanyika nchini humo katika muongo wa tisini.
Kagame ameeleza masikitiko yake kutokana na baadhi ya nchi kukataa kuwatia mbaroni washukiwa hao na kuwakabidhi kwa serikali ya Kigali.
Rais wa Rwanda ameongeza kuwa, nchi hizo zinapaswa kuelewa kuwa zinawajibika kuwakabidhi washukiwa hao wa mauaji ya kimbari. 
Wahutu wenye misimamo mikali waliwauwa Watutsi na Wahutu wenye misimamo ya wastani milioni moja katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini humo.


0 comments:

Post a Comment