Jaji Mostafa Hassan Abdullah wa mahakama ya jinai ya mjini Cairo, Misri
amejiondoa kusikiliza kesi ya mauaji iliyofunguliwa tena dhidi ya
dikteta wa zamani wa nchi hiyo Hosni Mubarak na kuamua kuihamishia kesi
hiyo kwenye mahakama ya rufaa. Jaji huyo aliyekuwa amepangiwa kusikiliza
tena kesi inayomkabili Hosni Mubarak, waziri wake wa zamani wa Mambo ya
Ndani Habib al-Adly pamoja na maafisa wengine wanne waandamizi wa
utawala wake amelazimika kutangaza uamuzi huo punde baada ya kuanza kesi
hiyo kufuatia fujo zilizozuka mahakamani kutokana na mawakili wa
familia za watu waliouawa katika vuguvugu la mapinduzi nchini Misri
kupinga uhalali wa jaji huyo kusikiliza kesi hiyo. Jaji Mostafa Abdullah
aliwahi kusikiliza kesi iliyojulikana kama Vita vya Ngamia na kuwatoa
hatiani washtakiwa wote waliotuhumiwa kuhusika na mauaji ya
waandamanaji. Kesi ya Hosni Mubarak itasikilizwa na mahakama ya rufaa
katika tarehe itakayotangazwa hapo baadaye. Katika kesi hiyo anakabiliwa
na mashtaka ya kufumbia macho mauaji ya waandamanaji zaidi ya 840
wakati wa kipindi cha siku 18 za wimbi la mapinduzi yaliyouangusha
utawala wake wa kidikteta. Mubarak alifikishwa mahakamani leo pamoja na
wanawe wawili wa kiume Alaa na Jamal wanaokabiliwa na mashtaka ya
ufisadi …/
Sikiliza Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment