10Jumaadal Aakhir,1434 Hijiriyah/ April 20,2013 Miyladiyah
Ehud Olmert Waziri Mkuu wa zamani wa utawala wa Kizayuni wa Israel
amekiri kwamba, mikakati kadhaa ya kigaidi iliyofanywa na utawala huo
dhidi ya miradi ya nyuklia ya Iran iligonga mwamba. Kwenye mahojiano
aliyofanyiwa na gazeti ka Kizayuni la Israel la 'Jerusalem Post' waziri
mkuu huyo wa zamani wa Israel amekiri kufeli njama za siri za utawala wa
Israel zilizokuwa na lengo la kukwamisha kabisa miradi ya nyuklia ya
Iran. Olmert amesema kuwa, kwa miaka kadhaa sasa Israel imekuwa ikifanya
mikakati ya kukwamisha miradi ya nyuklia ya Iran, lakini kwamba
Marekani ilipaswa kuchukua uongozi wa mikakati hiyo ya kuvuruga miradi
ya nyuklia ya Iran. Inafaa kuashiria hapa kuwa, katika miaka ya hivi
karibuni idadi ya wasomi na wataalamu kadhaa wa nyuklia wa Iran wameuawa
kigaidi na vibaraka wa utawala wa Kizayuni na mashirika ya kijasusi ya
nchi za Magharibi, amma miradi ya nyuklia ya Iran bado iko kwenye mkondo
uleule wa kuiwezesha Iran kujipatia nishati ya nyuklia kwa malengo ya
amani. Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia IAEA umethibitisha mara
kadhaa kwamba, hakuna dalili zozote zinazoonyesha kuwa Iran inataka
kutengeneza bomu la nyuklia.
Sikiliza Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment