Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Thursday 11 April 2013

Dk. Mwakyembe: Mkizidishiwa nauli semeni

SERIKALI imewataka abiria watakaopandishiwa nauli tofauti na viwango vipya vilivyotangazwa na serikali kuwa na ujasiri wa kutoa taarifa ili wahusika wachukuliwe hatua.
Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa jana na Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu nauli mpya za daladala na mikoani zinazoanza kutumika leo.
Alisema kuwa kumekuwepo na tatizo kubwa la wananchi kukaa kimya hata kama wakionewa kwa kutozwa kiwango cha nauli ambacho hakiendani na nauli halisi iliyopangwa na serikali kupitia Mamlaka ya Usafiri wa Nchini Kavu na Majini (SUMATRA).
Mwakyembe alisema mara kadhaa amekuwa akitembelea vituo vya daladala na kukuta abiria wakitozwa nauli ya sh 1,000 badala ya nauli halisi huku wakikaa kimya na kuishia kulalamika pembeni.
“Wananchi ni watu wa ajabu sana, hawana uthubutu hata kidogo wanapotendewa vitendo vya uonevu, badala yake wanasubiri serikali ndiyo iwasemee na kubaini matatizo yanayowakabili wao wakati wanaonyanyasika ni wao,” alisema.
Mwakyembe alitumia nafasi hiyo kuwataka wananchi kuwa na utayari na uthubutu wa kuwa wawazi.
 

0 comments:

Post a Comment