Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Friday 19 April 2013

'Darfur haiwezi kujitenga na Sudan'

                                      10Jumaadal Aakhir,1434 Hijiriyah/ April 20,2013 Miyladiyah
 Mshauri wa Rais Omar Hassan al Bashir wa Sudan amesema kuwa, eneo la Darfur haliwezi kujitenga na ardhi ya Sudan. Dakta Mustafa Othman Ismail amesema kuwa, sababu na vigezo vilivyopelekea Sudan Kusini kujitenga, havionekani katika eneo la Darfur. Dakta Mustafa Ismail ameongeza kuwa, hali ya kizazi, kiutamaduni, kidini na kilugha iliyoko Darfur inatofautiana kabisa na ile ya Sudan Kusini. Mshauri wa Rais wa Sudan amesema kuwa, wakazi wengi wa Sudan Kusini ni Wakristo, katika hali ambayo wakazi wengi wa jimbo la Darfur ni Waslamu na kwamba hiyo ndiyo sababu kuu inayozuia kujitenga wakazi wa eneo hilo na ardhi ya Sudan. Hali kadhalika Mshauri wa Rais al Bashir amesema kuwa, utawala ulioondolewa madarakani wa Kanali Muammar Gaddafi nchini Libya ulikuwa ukiyaunga mkono makundi ya waasi katika eneo la Darfur kwa kuyapa silaha na kuendeleza machafuko katika eneo hilo.

0 comments:

Post a Comment