11Jumaadal Aakhir,1434 Hijiriyah/ April 21,2013 Miyladiyah
Mechi kali ya kombe la
shirikisho baina ya Azam fc ya Tanzania dhidi ya timu ya jeshi la
Morroco AS FAR Rabat imemalizika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam
kwa matokeo ya suluhu pacha ya bila kufungana.
Katika mchezo huo timu zote
mbili zimekosa nafasi nyingi za kutia mpira nyavuni huku dakika za
mwisho waarabu wa Morroco wakijiangusha mara kwa mara kutaka suluhu
ugenini.
Azam FC imeshindwa kutamba
katika mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi Emile Fred kutoka Shelsheli
na endapo ingeshinda ingejiwekea mazingira mazuri ya kusonga mbele hatua
ya makundi.
Sasa Azam watakuwa na kibarua kizito huko kaskazini mwa Afrika wiki mbili zijazo kwani watahitaji ushindi tu na si vinginevyo.
Kama wawakilishi hao
watanzania watahitaji kujaribu bahati yao watahitaji kulazimisha suluhu
ugenini ili sheria itumike, lakini kama watahitaji kusonga mbele ndani
ya dakika 180 watalazimika kupata matokeo ya ushindi.
Katika dakika ya mwisho ya
mchezo huo nyota wa Azam Kipre Herman Tchetche alipiga bunduki moja
iliyogonga mtambaa panya na baada ya hapo mwamuzi Fred alipuliza kipenga
cha mwisho kuashiria ngoma imemalizika.
Akiongea baada ya mechi hiyo
kocha mkuu wa Azam fc, mwingereza Sterwat John Hall alisema ni matokeo
mabaya kwao kwani wanahitaji kujipanga vizuri mechi ya marudiano.
“Tumepoteza nafasi nyingi,
bahati haikuwa yetu lakini tunaweza kubadili matokeo tukienda kwao kwani
katika soka kila kitu kinawezekana”. Alisema Hall.
Kocha huyo aliongeza kuwa timu yake ilicheza vizuri na kwa umakini sana lakini bahati haikuwa yao kwa siku ya leo. Chanzo Mjengwa blog
Sikiliza Live
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment