Powered by Blogger.

Sikiliza Live

Saturday 13 April 2013

Ahoji wabunge wa Zanzibar kutohudhuria vikao TASAF

MBUNGE wa Viti Maalumu Tauhida Cassian Gallos (CCM), ameihoji serikali na kutaka kutoa maelezo kama ni makubaliano ya Serikali ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar kuwa wabunge wa Zanzibar wasihudhurie vikao vya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF) wakati wabunge wa Bara wanahudhuria.
Akiuliza swali la nyongeza bungeni jana, mbunge huyo pia alitaka kujua ni sababu gani ambazo zinasababisha wabunge kutoka Tanzania Zanzibar kutohudhuria vikao hivyo wakati wabunge wa Bara wanapata fursa ya kuhudhuria vikao  kama kawaida.
Katika swali la msingi, Tauhida alitaka kujua kwa upande wa Zanzibar mradi wa TASAF unasimamiwa na wizara gani.
Akijibu maswali hayo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu wa Bunge), Stephen Wasira alisema hakuna kizuizi chochote cha wabunge wa Zanzibar kutohudhuria vikao vya TASAF.
“Hakuna sababu yoyote ya wabunge kutohudhuria vikao vya TASAF, na kama hawahudhurii basi tutaangalia ni kwanini hawafanyi hivyo, lakini ninachoelewa ni kuwa wao ni wajumbe,” alisema Wasira.
Aidha alisema kwa upande wa Zanzibar mradi wa TASAF unasimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar.
Alisema Mkurugenzi wa uratibu katika ofisi hiyo ndie anayehusika na uratibu wa shughuli zote za TASAF chini ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar.
 

0 comments:

Post a Comment